0
Mshambuliaji Lionel Messi wa Barcelona ameibuka shujaa katika mechi ya El Clasico dhidi ya wapinzani wao kwenye soka la Spain klabu ya Real Madrid akifunga bao 2 katika ushindi wa bao 3-2.
Mechi hiyo ya ligi kuu Spain Laliga ilipigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu nyumbani kwa Real
Madrid. Casemiro alitangulia kuipatia Real Madrid bao la kuongoza dakika ya 28 lakini Lionel Messi akaisawazishia Barcelona dakika ya 33 bao hilo
akiwapiga chenga mabeki na kupiga shuti lililomshinda kipa wa Real Madrid Keylon Navas na kujaa wavuni kufanya timu hizo kwenda mapumziko matokeo yakiwa ni 1 -1.
Kipindi cha pili mnamo dakika ya 73 Ivan Rakitic aliipatia Barcelona bao la pili lakini James Rodriguez akaisawazishia Real Madrid akifunga bao dakika ya 86 lakini Messi aliwanyanyua mashabiki
wa Barcelona kwa kufunga bao la tatu ambalo lilimaliza kabisa mchezo.
Barcelona na Real Madrid wote wana pointi 75 katika msimamo.
Messi kwa mabao hayo mawili ni dhahiri kwamba amewafunga mdomo wale wote waliokuwa wanampondea eti ameshuka kiwango baada ya
kushindwa kuivusha timu yake hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Chapisha Maoni

 
Top