N'Golo Kante amewaachia manyoya Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovin na Alexis Sanchez na kuwa mchezaji bora wa
PFA N'Golo Kante ameshinda tuzo ya mchezaji borw wa PFA (Professional Footballers' Association) ya
mwaka 2016-17.
Kiungo huyo wa Chelsea amewapiku Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez katika kura kutoka kwa wachezaji wenzake Jumapili usiku kwenye hoteli ya Grosvenor mjini London.
Kante alishinda taji la Ligi Kuu akiwa na Liecester City mwaka jana, na anaweza kutwaa taji hilo tena akiwa na Chelsea msimu huu, atakuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji mtawalia akiwa
na klabu mbili tofauti.
Kante mwenye umri wa miaka 26, anatumikia msimu wa pili katika Ligi Kuu Uingereza baada ya kujiunga na Leicester akitokea Caen 2015, pia
aliisaidia Ufaransa kufika fainali Kombe la Euro 2016.
Kiungo wa Tottenham Dele Alli ameshinda tuzo ya mchezaji mdogo ya mwaka kwa msimu wa pili mfululizo, wakati nahodha wa zamani wa
Uingereza David Beckham akipokea tuzo ya heshima ya PFA kwa mchango wake kwenye soka.
Lucy Bronze wa Manchester City ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa kike, wakati Jess Carter wa Birmingham City akiwa mchezaji kinda wa kike
wa mwaka.
Chapisha Maoni