0
Lionel Messi ameweka rekodi nyingine ya Clasico baada ya kufunga kwa mara ya kwanza katika mechi saba dhidi ya Real Madrid Nyota wa Barcelona Lionel Messi ndiye kinara wa mabao kwenye mechi za Clasico za La Liga baada ya kufunga dhidi ya Real Madrid kwenye
uwanja wa Santiago Bernabeu.
Jitihada za Messi katika dakika ya 33
zilimwezesha kuikusanya vema pasi ya Ivan Rakitic na kuwatoka Luka Modric na Dani Carvajal kabla ya kumtungua Keylor Navas kwa shuti maridadi la yadi 12.
Hilo lilikuwa goli la 15 kwa Messi dhidi ya Real Madrid, na kufanikiwa kuvunja rekodi ya Alfred Di Stefano aliyetia kambani 14 enzi zake. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina tayari
ndiye kinara wa mabao Clasico katika michuano yote.
Kwa kuzifumania nyavu Messi alikomesha ukame mbaya wa mabao uliokuwa ukimkabili kwenye
mechi za Clasico. Alicheza mechi sita dhidi ya Madrid bila kufunga kabla ya mechi ya Jumapili.

Chapisha Maoni

 
Top