Manchester United ilijiongezea matumaini ya kuingia kundi la timu nne za kwanza baada ya kuwatandika Burnely 2-0
Wayne Rooney aliwafungia Manchester United likiwa ndilo bao lake la kwanza tangu mwezi Januari.
Hata hivyo Andre Gray, alikuwa na fursa nzuri ya kuifungia Burnley wakati wa kipindi cha kwanza wakati mkwaju wake ulipozuiwa na mlinzi Eric
Bailly.
Inamaana kuwa United inabaki nafasi ya tano katika Ligi kabla ya kukutana na hasimu wake Manchester City siku ya Alhamis.
Burnley nao wameshinda mara moja katika mechi 11 wakiwa katika nafasi ya 15.
Chapisha Maoni