limetangaza kuipoka Simba pointi
tatu na mabao matatu ambazo
ilipewa kutokana na mchezo wao
dhidi ya Kagera Sugar.
Wiki mbili zilizopita Simba ilipoteza
mchezo dhidi ya Kagera kwa
kufungwa mabao 2-1 kwenye
Uwanja wa Kagera mkoani Kagera
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara
lakini baadaye ilikata rufaa ikipinga
Kagera kumtumia mchezaji
Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na
kadi tatu za njano, ndipo ikapewa
ushindi huo kupitia Kamati ya Saa
71.
Mara baada ya kamati hiyo kuipa
Simba pointi Kagera ikaomba
kupitiwa upya kwa suala hilo na
nsipo TFF ikatangaza kuwa suala
hilo sasa litakuwa chini ya Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF ambayo ndiyo
imetoa maamuzi hayo.
Akizungumza na waandishi wa
habari juu ya uamuzi huo, Katibu
Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa
amesema kuwa kuna sababu
kadhaa zimechangia kuchukuliwa
kwa maamuzi hayo ambapo alisitaja
kuwa ni:
“Malalamiko ya Simba
hayakuwasilishwa kwa wakati
muafaka tangu mchezo
ulipochezwa, malalamiko yao
hayakuwa katika njia ya maandishi,
rufaa ya Simba haikulipiwa ada,
kikao cha Kamati ya Saa 72 kilikosa
uhalali kutokana na kuwashirikisha
watu ambao hawana uhalali wa
kuwa kwenye kikao.
“Kutokana na sababu hizo kamati
imeamua kufuta maamuzi
yaliyochukuliwa na Kamati ya Saa
72 na kurejesha matokeo kama
yalivyokuwa, pia kamati
imemuagiza katibu mkuu wa TFF
kuwapeweleka baadhi ya wajumbe
wa bodi ya ligi katika Kamati ya
Maadili ya TFF kwa kosa la kwenda
kinyume na kazi zao,” alisema
Mwesigwa.
Chapisha Maoni