0
Kamati ya Nidhamu ya TFF, imetangaza
kumfungia miezi 12 Msemaji wa Simba,
Haji Manara.
Pamoja na kufungiwa mwaka mmoja,
Manara amepigwa faini ya Sh milioni 9.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamy ya TFF, Wakili Jerome Msemwa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, Msemwa amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini Manara
amefanya utovu mkubwa wa nidhamu.

Chapisha Maoni

 
Top