katika nusu fainali ya Michuano ya
Azam Sports federation Cup
itakayofanyika Tarehe 29 mwezi huu
kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam, Hayo ni kufuatia droo ambayo
imefanyika mubashara Jumapili katika
studio Za AZAM.
Nusu fainali ya Pili ambayo itafanyika
tarehe 30 itazikutanisha Timu ya Mbao
ya Mwanza dhidi ya Mabingwa
watetezi wa Kombe hilo Yanga SC
Mchezo ambao utafanyika kwenye
uwanja wa CCM Kirumba Mwanza
ambapo Mbao atakuwa wenyeji.
Akizungumza wakati wa droo hio
meneja wa Azam FC Baruhani Muuza,
Amesema droo ya msimu huu
imekuwa na ubora kuliko ya mwaka
uliopita kwa kuwa imekuwa ya wazi
kwa wote kuona utaratibu wote.
-Droo ya msimu huu tumeamua iwe
mubashara, tumefanya hivi kwa
sababu tumeona ni kusota zaidi ili
kuimarisha kila mtu roho yake iweze
kuridhika" amesema meneja Huyo.
Waliohudhuria.
Waliohudhuria ni pamoja na Afisa wa
maendeleo TFF Jemedari Said, Iddi
Moshi ambaye ni Mchezaji wa zamani
wa Taifa Stars.
wawakilishi wa vilabu vyote vinne
ambapo Simba iliwakilishwa na Said
Tully ambaye ni mjumbe kamati ya
utendaji Simba, Hafidh Saleh meneja
Yanga, Phillip Alado Meneja AZAM na
Maselina Zephania mjumbe Mbao fc
Chapisha Maoni