0

Mchezaji wa Chelsea Nemanja Matic alifunga bao zuri kutoka mbali na kuisaidia timu yake kuinyamazisha Tottenham katika nusu fainali ya Kombe la FA katika uwanja wa Wembley.
Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyobasi kujikatia tiketi katika fainali ya kombe
hilo dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.
Willlian aliiweka mbele Chelsea kunako dakika ya sita kwa kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya
kuongeza la pili kwa njia ya penalti kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Harry Kane alikuwa amesawazisha kutoka kwa krosi iliopigwa na Christian Ericksen kwa Suprs
ambao walisawazisha tena kupitia bao la Delle Ali.
Mchezaji wa ziada Eden Hazard aliiweka Chelsea mbele kwa mara ya tatu kabla ya Matic kufunga
bao la nne na kuiweka kifua mbele Chelsea.



Chapisha Maoni

 
Top