ya Mwisho kutinga hatua ya nusu
fainali ya kombe la Shirikisho
Tanzania bara Maarufu kama Azam
Sports Federation Cup, mara baada ya
kuibuka na ushindi mnono wa mabao
3-0 dhidi ya Tanzania Prisons.
Mchezo huo wa mwisho wa Robo
Fainali umepigwa katika uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam na
kushuhudia mchezo safi kutoka kwa
Mabingwa wa Tetezi Yanga, ambao
walianza kulichachafya lango la
Tanzania Prisons na kupata bao
kunako dakika ya 15 kupitia kwa
Mrundi Amiss Tambwe.
Dakika ya 26 Tanzania Prisons
walifanya shambulizi kali ambapo
juhudi za mlinda mlango Beno
Kakolanya ziliweza kuzuia
wasisawazishe kwani alipangua kwa
ustadi na kutoka nje, na kuwa kona
tasa.
Dakika ya 40 kazi nzuri ya Wachezaji
wa Yanga ikazaa matunda baada ya
kupata bao la pili kupitia kwa
Mchezaji wa kimataifa wa Zambia
Obrey Chirwa aliyepiga bao safi kwa
njia ya Kichwa na kufanya Timu hizo
kwenda Mapumziko Yanga
wakiongoza kwa maba0 2-0.
Kipindi cha pili.
Kipindi cha pili kilianza kwa ulivu
huku kila timu ikijaribu kufuta makosa
ya kipindi cha kwanza Lakini dakika
mbili pekee ziliweza kuwafanya Yanga
kutumia Udhaifu wa Tanzania Prisons
kwa Simon Msuva kufunga bao la tatu
na la ushindi kaika dakika ya 47.
Baada ya bao hilo Tanzania Prisons
walianza kucheza kwa kulinda zaidi
kana kwamba haitoshi Yanga wao ndo
walizidi kulishambulia Lango la
Tanzania Prisons lakini hadi dakika 90
zinakamilika hakuna Timu iliyoona
Lango la Mwenzake.
Nusu fainali.
Kwa ushindi huo Yanga wanaungana
na Timu za Mbao FC, Simba SC na
Azam FC katika hatua ya Nusu Fainali
ya Kombe la Azam Sports Federation
ambayo droo yake itafanyika Jumapili
saa 9 Alasiri.
Chapisha Maoni